Salama Na BILLNASS SE6 EP57 | MJUKUU PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Katika pita pita zangu siku si nyingi nilimsikia mtu akimzungumzia mgeni watu wa wiki hii kwamba ni ‘Jay Z’ wa Bongo na si kwasababu kamuoa mmoja wa wasanii hodari wa kike na ambao wako juu ki muziki, ila pia akili yake ya kibiashara kwa kiasi kikubwa imemfanya yeye aone hivyo. Kwa ufahamu wangu niliambiwa na kushuhudia suala la maneno na mawazo ‘kuumba’. Pale mtu au watu wanapo kuona na ukichanganya na juhudi zako na nia na madhumuni ya wewe kutaka kufika pale basi mengine kutimia huwa ni suala la wakati tu. Hivyo pia ndivyo ambavyo mimi namuona Ndugu William Nicholaus Lyimo almaaruf Bill Nass. Mara yangu ya kwanza kukutana nae uso kwa macho ni miaka kama sita au saba iliyopita wakati nafanya kipindi cha Ngaz kwa Ngaz special edition. Ambacho mimi na Josh Murunga tulikua tunafanya ilikua kuwapa nafasi wasanii hodari kuwa ma host wa countdown hiyo ya ngoma zao kali 20 kwa wakati huo na kuzitolea maelezo yake. Kwa Bill Nass ilikua kama kumtafuta Kuku tu, yaani RAHISI sana. Alikua natural wataalam wanasema, kuanzia matamshi (haya wengi huwashusha hadhi kwa kiasi flani) mpaka swagg ambayo mtangazaji anatakiwa awe nayo kwake ilikua ipo. Kuvaa kwake, kuheshimu wakati na kuskiliza maelekezo na kisha kuyafanyia kazi ilikua 100, na mimi kwenye hili nilikua mtazamaji tu, kazi kubwa aliifanya Ndugu Josh akiwa kama Director. Yangu matumaini Bill Nass siku moja atataka kufanya kitu kama kile maana kitamfaa mno na itakua moja ya income zake nyingi ambazo anazo. Kwake yeye kuamua kumuoa mmoja ya wasanii hodari wa kike ambaye ana mashabiki wengi na pengine wengi wao ni wanaume nadhani lilikua si amuzi mdogo kwao wote wawili. Wawili hawa mahusiano yao yalikua hadharani kwa sote kuyaona na kuwa na maoni nayo. Kuanzia ku leak kwa video yao ya faragha mpaka mahusiano ya mkewe na Marehemu Ruge, kila kitu kilikua nje nje. Je haya yaliathiri au kuyajenga mahusiano yao kwa kiasi gani? Vipi kuhusu suala la Marehemu Godzilla ambaye kulikua na shutma kwamba alikua anauiga style yake na baadhi ya Radio zilikua zinampa nafasi yeye ili kumficha Zilla? Na je suala la kifo chake ambalo lilimleta yeye karibu na mtoto wa Zilla? Hii ilikua inamsumbua vipi wakati watu wanasema hivyo? Na je alikua anaona jinsi ambavyo ilikua inamsumbua Zilla? Ukiachana na muziki Nenga pia ni mfanyabiashara mzuri tu ambaye amekua akitumia jina lake ipasavyo ili kuweza kujitengenezea kipato cha pembeni ambacho ni cha uhakika zaidi kuliko mziki ambao anafanya. Nna uhakika na yeye anajua kwamba ana uhakika wa kuuza electronics zaidi kwa mara nyingi kuliko uhakika wa kuwa na hit song nyingi kwa mwaka. Na hiyo haimaanishi kama yeye si msanii HODARI ila zaidi kwenye suala la wimbo kuwa mzuri lakini watu wasiupokee kama matarajio yanavyokua. Humu pia tulichambua kiasi kuhusu jina lake ambalo amelirithi. Majukumu, biashara, mapenzi, urafiki, usia na familia. Ningependa u enjoy kama ambavyo sisi tu enjoy wakati tunaongea. Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬ ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬ GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible & Msam...   Follow: Twitter:   / yahstonetown   Instagram:   / yahstonetown   Facebook:   / yahstonetown   Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Salama Na BILLNASS SE6 EP57 | MJUKUU PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
▶︎

Salama Na BILLNASS SE6 EP57 | MJUKUU PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na LULU DIVA SE6 EP61 | UKIPATA KINYAKUE… PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
▶︎

Salama Na LULU DIVA SE6 EP61 | UKIPATA KINYAKUE… PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

MY REPLY SHOW W/ BILLNASS S02EP02 | BILLNASS AJIBU MASWAL YOTE MAGUMU YA FANS WAKE | MY REPLY SHOW
▶︎

MY REPLY SHOW W/ BILLNASS S02EP02 | BILLNASS AJIBU MASWAL YOTE MAGUMU YA FANS WAKE | MY REPLY SHOW

Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1
▶︎

Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1

PART II: BILLNASS: "BOSS RUGE ALINIPIGIA SIMU, NAMBA NAIJUA, NILIM-BLOCK NANDY"
▶︎

PART II: BILLNASS: "BOSS RUGE ALINIPIGIA SIMU, NAMBA NAIJUA, NILIM-BLOCK NANDY"

HASSAN MWAKINYO BAADA YA PAMBANO/PESA NILIYOPATA HAPA LEO ITANISAIDIA KULIPIA KODI YA NYUMBA
▶︎

HASSAN MWAKINYO BAADA YA PAMBANO/PESA NILIYOPATA HAPA LEO ITANISAIDIA KULIPIA KODI YA NYUMBA

MWANAMKE ALIYE MTEKA MTOTO SHULENI NA KUTAKA ALIPWE  MILIONI 20,AKAMATWA NA MTOTO  TABORA
▶︎

MWANAMKE ALIYE MTEKA MTOTO SHULENI NA KUTAKA ALIPWE MILIONI 20,AKAMATWA NA MTOTO TABORA

🔴#LIVE_ GOD YANGA ATAMBA USHINDI "KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE ! MWAMNYETO HANA BAYA AMETUHESHIMISHA
▶︎

🔴#LIVE_ GOD YANGA ATAMBA USHINDI "KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE ! MWAMNYETO HANA BAYA AMETUHESHIMISHA

SISI ILEWE | 2026 Latest Nigeria Movie - Ego Nwosu, Kunle Remi, Kamo State
▶︎

SISI ILEWE | 2026 Latest Nigeria Movie - Ego Nwosu, Kunle Remi, Kamo State

Salama Na TID SE6 EP07 FULL SHOW|NYOTA YAKO PART 1|SendTip MPESA LIPA NO 5578460
▶︎

Salama Na TID SE6 EP07 FULL SHOW|NYOTA YAKO PART 1|SendTip MPESA LIPA NO 5578460

ASMR ✨ Starting My Fantasy Shop in Winkeltje 💰 Close Up Whispering
▶︎

ASMR ✨ Starting My Fantasy Shop in Winkeltje 💰 Close Up Whispering

Salama Na OSCAR OSCAR SE6 EP39 | UALIMU?! SI WITO!! PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
▶︎

Salama Na OSCAR OSCAR SE6 EP39 | UALIMU?! SI WITO!! PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

BILLNASS : NIMEISHI GHETTO ALILOKAA GODZILLA, KWA WANA HIPHOP SIKOSI NAMBA 2 AU 3, NIMEVUNJIKA MOYO
▶︎

BILLNASS : NIMEISHI GHETTO ALILOKAA GODZILLA, KWA WANA HIPHOP SIKOSI NAMBA 2 AU 3, NIMEVUNJIKA MOYO

HECHE AMKABA KOO WAZIRI MWIGULU | KAZI YAKO SIO KUTATUA MIGOGORO YA NDOA | FANYA KAZI YAKO WAZIRI
▶︎

HECHE AMKABA KOO WAZIRI MWIGULU | KAZI YAKO SIO KUTATUA MIGOGORO YA NDOA | FANYA KAZI YAKO WAZIRI

Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1
▶︎

Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1

HARMONIZE "Hakuna Msanii asiyemshabikia ALIKIBA/Awachana Wachambuzi"
▶︎

HARMONIZE "Hakuna Msanii asiyemshabikia ALIKIBA/Awachana Wachambuzi"

Mkasi - SO6E03 With Millard Ayo
▶︎

Mkasi - SO6E03 With Millard Ayo

SURAH AL KAHF سورة الكهف | BEAUTIFUL CALMING RECITATION TO SOOTHE YOUR HEART | Habibullah TV
▶︎

SURAH AL KAHF سورة الكهف | BEAUTIFUL CALMING RECITATION TO SOOTHE YOUR HEART | Habibullah TV

EXCLUSIVE: MC GARA B - NILIUMWA SANA NILIFIKIA KUWA KICHAA/MAMA YANGU ALINIKATIA TAMAA.
▶︎

EXCLUSIVE: MC GARA B - NILIUMWA SANA NILIFIKIA KUWA KICHAA/MAMA YANGU ALINIKATIA TAMAA.

Morara Kebaso | In Conversation w\Chaxy #6
▶︎

Morara Kebaso | In Conversation w\Chaxy #6