MPANDA: DIWANI AKATAA GREDA KUKANYAGA KWENYE KATA YAKE KAMA HATAPATA KM 7 ZA BARABARA.

Diwani Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda akataa Greda kukanyaga kwenye Kata yake kama hatapata Km 7 za barabara alizoahidiwa. Diwani wa Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Maiko Kamande ameitaka Wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) kutopeleka greda kwa ajili ya kuchonga barabara katika kata hiyo kama hawataeleza sababu za awali kupanga kukarabati barabara zenye Km 7 na sasa ibaki Km 1. Kamande ametoa msimamo huo leo Januari 31,2023 baada ya taarifa ya TARURA iliyowasilishwa na Menejea wa TARURA Mpanda, Mhandisi Kahoza Joseph katika kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Mpanda na kuonyesha Kata hiyo inatachongewa barabara ya Km 1. Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry amemtaka Meneja TARURA kukutana na Diwani huyo na kupitia makablasha upya ili ifahamike ni Km 7 au 1 kuondoa sintofahamu hiyo.