Maisha Ya Zuchu Kabla Ya WCB : "Nilitaka Kuwa Mwanasheria" | SALAMA NA ZUCHU PART 1

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Kuna usemi mmoja unaenda kama hivi, kulea mimba si kazi ila kazi ni kulea mtoto, tafsiri yangu naamini mhenga hapo alikua anatuambia kazi pengine inaanza baada ya kupata kazi, tunaelewa jinsi gani ambavyo kupata kazi huwa ni kazi. Tena kazi yoyote, haijalishi kama ni ya upishi au ulinzi au ufundi au hata u daktari, mi nawajua madaktari kadhaa ambao nao pia wanapata shida kupata hizo kazi. Na baada ya kupata shida zote hizo wakati wa kutafuta kazi basi kazi halisi huanza pale unapoipata sasa hiyo kazi yenyewe. Kazi ya Zuchu ilianza kabla hajaipata hiyo kazi yenyewe na ilikua kazi haswa kuipata na Mama yake Bi Khadija Kopa ndo alikua kinara kwenye hiyo connection ambayo Binti yake alikua anaitaka ili aweze kuwa msanii wa Diamond, na hayo ndo yalikua maneno yake hasa, toka alivyorudi kutoka Nigeria kwenye mashindano ya kusaka vipaji na alikua hajielewi elewi kwa kiasi flani ni kitu gani alikua anataka kufanya na kama basi kutakua na la kufanya inabidi liwe kutoka WCB na sio sehemu nyengine yoyote na agulia nini kilitokea? WCB aliipata na kilichokua kinatakiwa baada ya hapo ni UVUMILIVU wa HALI YA JUU. Kwenye vitabu vyangu vyote Bi Zuhura Othman Soud ndo muandishi wangu BORA wa KIKE kuwahi kutokea katika kizazi chetu hiki cha Bongo Flava, na naweza sema hivyo wakati wowote iwe usiku au mchana, kipaji hicho ndicho kilichonifanya mimi nistaajabu sana na kutaka kuongea nae na kumuuliza yote yale ambayo nilikua nataka kumuuliza, ingawa humo humo nilikua nishajijibu kutoka kwenye historia ya familia atokayo ingawa hiyo haikutakiwa ndo iwe lazima, lazima mtoto wa Khadija Kopa na Othman Soud awe muandishi mzuri maana wazazi wake wamejaa vipaji tena na Baba yake ndo muandishi mkubwa wa nyimbo nyingi za Mama yake zilizowahi kuvuma. Kwa umri wake wakati mwengine hujiuliza kajuaje haya maneno yote, anajua maana yake hii? Kasikia wapi hili neno au pengine je huwa anamfikiria Mama yake (ambaye ndo kipenzi chake na ndo amemlea) wakati anaandika hii? Anaona aibu? Je huwa wanaongelea hayo mashairi wanapokua wawili tu? Mazungumzo huendaje? Sasa turudi kwenye kazi hiyo ya kuanza kuifanya baada ya kuipata sasa WCB, ukiachana na msoto mrefu alopitia, WCB wenyewe walikua waangalifu sana kwenye mipango ambayo ilikua ikiandaliwa kwaajili yake, yeye ndo msanii wa KWANZA wa KIKE kuwahi kutokea kwenye label kwahiyo ukichana na kipaji pia uwekezaji wa hali ya juu ulitakiwa ufanyike and boy they did that. Toka single yake ya kwanza mpaka wakati naandika hii Zuchu hakuwahi kuwa na kazi chafu, album yake ya kwanza alotoka nayo ya I am Zuchu ilikua na nyimbo 7 ambazo zote zilienda kufanya vizuri, na mpaka leo kila wimbo ambao anaachia ni wa moto, tukisema namba moja nadhani namba zake pia zinasema hivyo za kila sehemu, hakuna chumvi yoyote ndani yake. Vipi sasa anaweza ku maintain hii schedule yake ilojaa mambo kuanzia asubuhi mpaka usiku? Kutoka Jumatatu mpaka Jumapili? Je ana muda kwaajili yake? Ana mpenzi? Mipango yake je? Endelevu? Vipi hizi title ambazo tunampa anazichukuliaje? Kuna pressure yoyote? Na kuhusu familia je? Kuna pressure yoyote kwenye baadhi ya mambo na maamuzi? Na kwenye label nako? Watu na furaha na kazi yake? Kwa kuanzia msimu wetu wa TANO nadhani introduction ya Ms Zuchu inatufaa sana na yangu matumaini uta enjoy pia. Asante kwa support ya toka siku ya kwanza ulipoanza kutupa macho na masikio yako. You’re the best, nakukumbusha tu kwamba mengi yajayo yatakufurahisha In Shaa Allah maana kazi ndo kwaanza imeanza. Love, Salama

Sheikh Kipozeo: "Sisi Ni Watu Wa Mwisho Wa Dunia, Kiama Bado" | SALAMA NA SHEIKH KIPOZEO PT 2
▶︎

Sheikh Kipozeo: "Sisi Ni Watu Wa Mwisho Wa Dunia, Kiama Bado" | SALAMA NA SHEIKH KIPOZEO PT 2

Zuchu : "Nilipeleka Nyimbo Kama Tano, Diamond Alizikataa Zote" | SALAMA NA ZUCHU
▶︎

Zuchu : "Nilipeleka Nyimbo Kama Tano, Diamond Alizikataa Zote" | SALAMA NA ZUCHU

January reset (weightloss journey,visionboard & self love) part 1
▶︎

January reset (weightloss journey,visionboard & self love) part 1

KIJANA MKOROFI AMTUKANA BINTI WA KISHUA,BILA KUJUA NI MTOTO WA BOSS WAKE
▶︎

KIJANA MKOROFI AMTUKANA BINTI WA KISHUA,BILA KUJUA NI MTOTO WA BOSS WAKE

Kanumba alikuwa zaidi ya Daraja la kazi kwao? (A list S01 Ep03)
▶︎

Kanumba alikuwa zaidi ya Daraja la kazi kwao? (A list S01 Ep03)

MASHALOVE AFUNGUKA MADUDU YA GIGY MONEY/AMEJILIPIA MAHARI YA HARUSI/ZUCHU HAMPENDI/SIWEZI KUMROGA
▶︎

MASHALOVE AFUNGUKA MADUDU YA GIGY MONEY/AMEJILIPIA MAHARI YA HARUSI/ZUCHU HAMPENDI/SIWEZI KUMROGA

ANAPOISHI NGOMA NAGWA/NILIKUA MWIZI/ALIWEKA BONDI NYUMBA KWA LAKI TANO/MKE WANGU NDIO ADUI YANGU
▶︎

ANAPOISHI NGOMA NAGWA/NILIKUA MWIZI/ALIWEKA BONDI NYUMBA KWA LAKI TANO/MKE WANGU NDIO ADUI YANGU

FULL SHOW YA ZUCHU DAKIKA 50 BILA KUCHOKA YANGA DAY KWA MKAPA | D VOICE AINGIA KIFALME NA SINGELI
▶︎

FULL SHOW YA ZUCHU DAKIKA 50 BILA KUCHOKA YANGA DAY KWA MKAPA | D VOICE AINGIA KIFALME NA SINGELI

WATOTO wa JACKIE CHAN wanavyomnyima usingizi, waonekana aibu kwa Familia na kunyimwa urithi wa $400m
▶︎

WATOTO wa JACKIE CHAN wanavyomnyima usingizi, waonekana aibu kwa Familia na kunyimwa urithi wa $400m

Dore amayeri Korea ya ruguru yigishije Iran none bigaranzuye USA,Trump na Netanyahu sibariguhuza
▶︎

Dore amayeri Korea ya ruguru yigishije Iran none bigaranzuye USA,Trump na Netanyahu sibariguhuza

ICU-CHUMBA CHA UMBEA | EXCLUSIVE: MBOSSO AFUNGUKA, BIFU LAKE NA ZUCHU, NIMEONDOKA WCB KISA ZUCHU
▶︎

ICU-CHUMBA CHA UMBEA | EXCLUSIVE: MBOSSO AFUNGUKA, BIFU LAKE NA ZUCHU, NIMEONDOKA WCB KISA ZUCHU

Valentine get away ❤️🌹😍
▶︎

Valentine get away ❤️🌹😍

Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1
▶︎

Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1

MADAM RITA, NJIWA UCHWARA NA KASUKU UCHWARA WAFIKA BSS | HUYO NI SPARROW
▶︎

MADAM RITA, NJIWA UCHWARA NA KASUKU UCHWARA WAFIKA BSS | HUYO NI SPARROW

ZUCHU AFUNGUKA KUWA  MJAMZITO/NIMEPOTEZA MUDA MREFU WASAFI/DIAMOND/KHADIJA KOPA/AZINDUA DARASA
▶︎

ZUCHU AFUNGUKA KUWA MJAMZITO/NIMEPOTEZA MUDA MREFU WASAFI/DIAMOND/KHADIJA KOPA/AZINDUA DARASA

BILIONEA WA MA-RANGE, ALIYEACHA KAZI YA POLISI AWE DEREVA, ALIVYOKIMBILIA UINGEREZA, WAZUNGU WAMTII.
▶︎

BILIONEA WA MA-RANGE, ALIYEACHA KAZI YA POLISI AWE DEREVA, ALIVYOKIMBILIA UINGEREZA, WAZUNGU WAMTII.

MH! ZARI AFUNGUKA MAPYA MAHUSIANO YAO NA DIAMOND/UPENDO UMEZIDI SANA TUMEJUANA
▶︎

MH! ZARI AFUNGUKA MAPYA MAHUSIANO YAO NA DIAMOND/UPENDO UMEZIDI SANA TUMEJUANA

JARED OKODE aka DEFAO: I Owned My First Shop in Class 7 || Lessons at 30 with Dr. Ofweneke
▶︎

JARED OKODE aka DEFAO: I Owned My First Shop in Class 7 || Lessons at 30 with Dr. Ofweneke

Day 2 with my family | In My Diary by Fahyvanny
▶︎

Day 2 with my family | In My Diary by Fahyvanny

NYUMBANI KWA MASHAVU WA KOMBOLELA/GHOROFA LA MAANA/NAISHI NA MTOTO WANGU/BABA YAKE AMENIUMIZA SANA
▶︎

NYUMBANI KWA MASHAVU WA KOMBOLELA/GHOROFA LA MAANA/NAISHI NA MTOTO WANGU/BABA YAKE AMENIUMIZA SANA