UGONJWA WA SONONA: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia
Katika video hii inazungumza kuhusu sababu, dalili, matibabu, namna ya kuzuia, matarajio baada ya matibabu ya UGONJWA WA SONONA, endelea angalia mpaka mwisho kujifunza Sonona (Depression) ni hali ya kuhisi huzuni, kushuka moyo na kukosa furaha. Wengi wetu tunajihisi huzuni au kukosa furaha kwa wakati mmoja au mwingine kwa muda mfupi. Lakini kwa mgonjwa wa sonona, hisia hizi zinakuwepo muda wote na kwa muda mrefu. Ugonjwa wa sonona ni tatizo la kihisia, mgonjwa anahisi huzuni mwingi na hasira. Mfadhaiko wa aina hii unavuruga kabisa mfumo wa maisha ya kila siku wa mgonjwa. Je! Nini dalili za sonona? • Unapokuwa na sonona: o Unakuwa na hali ya msononeko au hasira wakati wote o Unapoteza hamu ya kufanya shughuli au mambo aliyokuwa akiyafurahia. o Hapati usingizi au analala sana o Anashindwa kula chakula kabisa au anakula muda wote – hii inaweza kusababisha akapungua sana uzito au kuongezeka uzito o Anajihisi Uchovu na kukosa nguvu – hawezi hata kutoka kitandani o Mgonjwa anajihisi kutokuwa na thamani yoyote, anajichukia, na anajihisi mwenye hatia o Hapendi kufanya jambo lolote na anaepuka kufanya shughuli za kawaida o Anajihisi kukata tamaa na bila msaada o Anapata mawazo ya kifo au kujiua mara kwa mara o Kutokujiamini ni swala la kawaida kwa mgonjwa wa sonona. Anaweza pia kuwa na hasira za ghafla na anakosa raha hata anapofanya mambo yanayopasa kumfurahisha – hata kujamiiana hakumfurahishi. o Watoto wenye sonona wanaweza wasiwe na dalili sawa na watu wazima. Angalia mabadiliko kwenye kazi za shule, usingizi, na tabia. Kama unashuku mwanao ana ugonjwa huu, ni muhimu kuongea na mtoa huduma wa afya. Sonona husababishwa na? • Baadhi ya watu wanarithi jeni zinazoongeza hatari ya kuwa na ugonjwa wa sonona. Tabia unazojifunza nyumbani pia zinaweza kuchangia watu wa familia fulani kuwa na sonona. Watu wanaozaliwa na jeni hizi wanaanza kuwa na ugonjwa huu baada ya tukio la kuhuzunisha linaloongeza msongo wa mawazo. • Kutumia pombe kupita kiasi au kutumia madawa ya kulevya kunaweza kusababisha sonona • Mgonjwa ya muda mrefu kama kansa, ukimwi, maumivu ya muda mrefu au magonjwa yanayosababisha ukose usingizi. • Matukio magumu ya kimaisha pia yanaweza kusababisha ugonjwa wa sonona: o Unyanyaswaji au kutelekezwa o Kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi o Kifo cha mke, mme, mtoo, jamaa au rafiki kipenzi o Talaka, hii ni pamoja na talaka kwa mzazi o Kufeli mitihani au kurudia darasa o Kuugua kwa mwanafamilia o Kupoteza kazi o Kutengwa na jamii (hasa kwa wazee) Wakati gani utafute matibabu ya haraka? • Ukihisi au ukiwa na mawazo ya kujiua, mwambie mtu uliyekaribu yako au nenda katika kituo cha afya kilicho karibu yako. • Mwone daktari kama: o Unasikia sauti ambazo hazipo au watu wengine hawazisikii o Unalia lia kila mara bila sababu yoyote o Sonona imeathiri uwezo wako wa kufanya kazi, kusoma shule, au kuishi vyema na familia kwa zaidi ya wiki 2 o Kama unadhani moja ya dawa unazotumia zinakusababishia dallili za sonona. USIBADILI au USIACHE kutumia dawa yoyote bila kuzungumza na daktari o Unafikiri unapaswa kupunguza kunywa pombe, mwanafamilia au rafiki amekuomba kupunguza unywaji wa pombe, unahisi hatia kuhusu kiasi cha pombe unachokunywa, au unakunywa pombe asubuhi sana Utambuzi • Daktari ataongea na wewe kuhusu historia yako ya kiafya na familia yako, atakufanyia uchunguzi wa mwini na kuagiza vipimo kadhaa kama ikihitajika • Daktari atagundua ukali wa ugonjwa wako (sonona inaweza kuwa kadri, wastani, au kali) na kisha atakueleza mpango wa matibabu. Uchaguzi wa matibabu Watu wengi wanaoishi na ugonjwa wa sonona, wanasema – ugonjwa wa sonona ni zimwi unalopambana nalo kila siku unapoamka mpaka unapoenda kulala – ni zito – na unahitaji msaada kulibeba. Matibabu ya sonona yanategemea dalili ulizonazo – kama dalili ni za kadri– daktari anaweza kukupatia ushauri na kukufunza namna ya kujitunza mwenyewe ukiwa nyumbani – tutayazungumza mambo haya muda mfupi ujao. Lakini kwa watu wenye Sonona ya wastani au kali – wanapatiwa dawa za kudhibiti sonona na tiba maongezi ''talk therapy''. Daktari anaweza kuamua kukupeleka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya akili kama sonona yako ni wastani au kali, au kama matibabu anayokupatia hayasaidii. Emmanuel Mniko #mniko #wikielimu @wikielimu

Dhjami i barkut në Menopauzë / Dr. Balili iu drejtohet grave: Hani…

Fahamu kuhusu ugonjwa wa sonona dalili na matibabu yake

“Diabeti i tipit 2 zgjidhet brenda javës, ja ushqimet”, flet këshilluesi i mjekësisë holistike

KIUNGULIA: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

Mazoezi bora kwa maumivu ya shingo | Best Exercises for Neck pain in Swahili Kenya

ایا قهوه واقعا به درمان کبد چرب کمک میکنه؟ بررسی آخرین مطالعات با دکتر بابک جمالیان

CHIA SEEDS IKIRIBWA GITANGAJE ! NI UMUTI W'AKATARABONEKA KU BUZIMA BWA MUNTU .

MAPIGO YA MOYO KWENDA MBIO: sababu na Nini cha kufanya

Niba utwite ukeneye iyi ntungamubiri! Vit B ifasha kurema ubwonko bw’umwana, umutima n’amaraso.

This is what causes fibroids!

UFAHAMU UGONJWA WA KOO, DALILI NA MATIBABU YAKE, "UGORO UNAWEZA KUSABABISHA SARATANI" - DR. KIMWAGA

DEGEDEGE: Sababu, huduma ya Kwanza

10 Behaviors That Are Actually Signs of Mental Illness

DALILI: Ugonjwa wa afya ya akili ujulikanao kama #Sonona (Depression) na dalili zake! #SAIKOLOJIA

AfyaCheck S02EP11 23July2014 Magonjwa ya zinaa (Kaswende)

The Full Truth About Herpes

Flohsamen, Leinsamen und Chia - wer GEWINNT?

KUMTELEKEZA MTOTO (Neglect): Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

UPUNGUFU WA MAJI MWILINI: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

