Meneja wa Huduma za Taasisi - PPAA, Bw. Paschal Kajuna

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeendesha mafunzo ya siku moja kwa vijana, wafanyabiashara, wakandarasi, watoa huduma na wadau wa ununuzi wa umma pamoja na makundi maalum wa mkoa wa Ruvuma na kuwasihi kutumia kikamilifu fursa zinazopatikana katika zabuni za Umma.