NENO LA SIKU | Mathayo 28 | Maombi Ya Kushinda Uzushi | Isaac Javan
Leo tunamaliza kusoma kitabu cha Mathayo, na tunaenda kufanya maombi ya kushinda uzushi. Katika maisha tunayoishi, hakuna jambo baya kama kuzushiwa maneno ya uwongo na watu wakaamini. Kuna watu wamekata tamaa ya maisha kwa sababu ya kuzushiwa maneno ya uwongo. Kuna watu wamepoteza marafiki kwa sababu ya kuzushiwa maneno ya uwongo. Kuna watu wametengana na wapendwa wao kwa sababu ya uzushi. Kimsingi, uzushi ni kitu kinachoweza kuharibu maisha ya mtu. Lakini habari njema ni kwamba, YESU alishatuandalia majibu ya tatizo hili. Damu yake ilipomwagika, ilitufungulia njia ya kutembea katika ushindi ikiwa ni pamoja na kushinda roho za uzushi ziharibuzo. Katika maombi ya leo, tunaenda kuomba YESU atufungue na kutuweka huru. Mahali popote ambapo uliwahi kuzushiwa jambo baya la uwongo, siku ya leo YESU anaenda kukuponya na pia anaenda kukurudishia vyote ulivyopoteza na anaenda kukupa heshima katika maisha yako. Kwa hiyo utakapokuwa unaomba, nakutia moyo ufanye maombi kwa kumaanisha, na utauona mkono wa BWANA ukikupigania na kukushindia. Mwisho kabisa, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kuungana nami katika usomaji huu wa biblia pamoja na maombi. Asante kwa wote uliowashirikisha waungane nasi katika maombi haya. Hongera sana kwa kufanikisha kusoma neno la Mungu kutoka kitabu chote cha Mathayo. Nakutia moyo, endelea kurudia maombi tuliyokwishafanya, mpaka uone umepata matokeo mazuri. Baada ya siku saba tutaendelea na kitabu cha Marko. Mpaka hapo tutakapoonana tena, nakuacha na amani ya YESU. Damu ya YESU ikulinde na inene maneno mazuri kwa ajili yako. YESU akuonekanie na akuvushe katika mambo yako yote. YESU akupiganie na akutetee katika kila jambo linalogusa maisha yako. Neema ya KRISTO YESU isikupungukie. YESU akupiganie na akuweke panapo nafasi. Mungu Roho Mtakatifu akutie nguvu unapoendelea kurejea maombi tuliyokwisha fanya. Utunzwe na damu ya YESU tangu sasa na siku zote. Amen

NENO LA SIKU | Marko 1 | Maombi Ya Kufungua Mbingu | Isaac Javan

KUOTA UNAOMBA USINGIZINI. WEWE NI M2 MWENYE UWEZO MKUBWA SANA WA KUZUIA MATUKIO. PART 2 Subscribe

BWANA YESU Niponye | Isaac Javan

Heri Wamtumainio Bwana//Liseme//Natamani Nikuone//Natamani Kutembea Nawe// POWERFUL SWAHILI WORSHIP

NAMNA YA KUONDOA AIBU || ASKOFU MKUU STEVIE MULENGA

NENO LA SIKU | Matendo 17 | Maombi Ya Kumtafuta Mungu | Isaac Javan

Hillsong Worship Songs 2026 Collection, Top Christian Worship Music, Morning Worship Songs Playlist

MAOMBI YA KUSHINDA ROHO ZA MAGONJWA

WORD OF THE DAY | Acts 26-28 | Prayer For God's Help | Isaac Javan

KWA NINI NIKIOMBA NASHAMBULIWA?

KULIGUNDUA KUSUDI LAKO NA KULIISHI (JOEL NANAUKA)

NENO LA SIKU | Luka 1 | Maombi Ya Kushinda Roho Ya Utasa | Isaac Javan

USINIPITE BWANA - DEEP RELAX SWAHILI WORSHIP SONGS

TAREHE:::22/4/2026:::MGUSE MUNGU HIVI UTAONA MATOKEO YA MAOMBI YAKO || PR.DAVID MMBAGA

NENO LA SIKU | Matendo 20 | Maombi Ya Kushinda Roho Za Ajali | Isaac Javan

Morning Worship Songs 2026 ✝️ Best Praise & Worship Music | Daily Peace Playlist

USIKU MWEMA | Isaac Javan

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING - 24 JUNE 2026

NAFASI YA MAVAZI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

